-->

Recent

Zijue Faida za karoti kwa afya yako.

karoti hulimwa karibia kila sehemu hapa duniani .Wanahistoria wanaamini kwamba karoti zililimwa na wagiriki na waroma .
Kuna karoti za rangi mbali mbali , ambazo ni rangi ya orange , pinki , njano,nk.


Carrot Nutrition Facts




Faida za karoti kwa afya yako.


Karoti ni nzuri kwa ajili ya uwezo wa macho yetu, kwasababu zina kiwango kikubwa sana cha vitamini A, Ukweli ni kwamba karoti zina pigment ziitwazo beta carotene ambazo  hugeuza kuwa vitamini A katika ini. Kwasabau beta carrotente haiwezi kutengenezwa kwenye miili yetu hivyo basi tunalazimika kupata kupitia chakula .


Maalum kwaajili ya kuzuia mionzi ya utravioleti , Pia karoti zianafanya kazi kubwa sana katika kuzuia magonjwa ya moyo na kiharusi ,Pia huzuia maambukizi kwenye vidonda, Pia husaidia kuifanya ngozi yako iwe yenye afya na kupendeza muda wote.


Karoti zina madini ya calcium, phosphorus, na magnesium ambayo husaidia katika kujenga mifupa yenye nguvu na afya ya mfumo wa neva. Matumizi ya Calcium ni muhimu kwa afya ya misuli ya moyo , phosphorus ni katika kulainisha ngozi na uimara wa meno, nywele na mifupa wakati magnesium ni husaidia katika maendeleo ya akili, mmengenyo wa mafuta.


Tafiti mbali mbali kuhusu karoti


Utafiti uliofanyika mwaka 2011,ulikuja na uthibisho kwamba kemikali zilizopo kwenye juisi ya karoti husaidia kutibu baadhi ya kansa  ikiwa ni pamoja na leukemia kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha antioxidants,Karoti pia imetajwa hasa katika orodha ya vyakula ambavyo hufanya kazi kubwa ya kupunguza hatari ya kansa ya kibofu cha mkojo kutokana na utafiti uliofanya na San Diego Medical Center


Wakati wengi wetu tunafahamu kwamba mboga mbichi huwa na virutubisho kwa wingi, ya kushangaza, uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha kwamba kupikia husaidia kuongeza faida ya afya ya karoti. 


HITIMISHO
karoti zinakiwango kikubwa sana cha beta carotene  kuliko aina nyingine ya mboga mboga au matunda hivyo basi husaidia kuzuia seli zinazopelekea kansa, 
Naamini kwamba kula chakula vizuri uwiano ni njia bora ya kudumisha afya yako.


Imeandaliwa na nutrition expert.

Disqus Comments

Main Slider